Utajiri wa mafuta waifanya nchi hii kujihisi kuwa na hatia

Watu wengi wa Norway wanahisi kana kwamba wana hatia, kulingana na Elisabeth Oxfeldt.

Profesa wa fasihi ya Skandinavia katika Chuo Kikuu cha Oslo anasema matajiri wa Norway wanazidi kulinganisha maisha yao ya kifahari na yale ya watu wanaotatizika, haswa ng’ambo.

“Tumeona kuibuka kwa masimulizi ya watu kuhisi ni kana kwamba wana hatia kuhusu maisha yao ya starehe katika ulimwengu ambao wengine wanateseka,” anasema.

Kwa sababu ya akiba yake kubwa ya mafuta- kubwa zaidi barani Ulaya baada ya Urusi, Norway ni moja ya nchi tajiri zaidi ulimwenguni.

Nguvu ya uchumi wake, kama inavyopimwa kwa kila mwananchi, ni karibu mara mbili ya ile ya Uingereza, na kubwa zaidi kuliko ile ya Marekani.

Norway hata fedha za ziada katika bajeti – mapato yake ya kitaifa yanazidi matumizi yake. Hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine mengi, ikiwa ni pamoja na Uingereza, ambayo inalazimika kukopa pesa ili kufidia pengo katika bajeti yake.

Prof Oxfeldt ni mtaalamu wa jinsi vitabu, filamu na vipindi vya televisheni vya Skandinavia vinavyoakisi utamaduni mpana wa wakati wao. Anasema anazidi kuona watu hawa wakichunguza hisia za hatia ya utajiri wa Norway.

“Kwa kutazama fasihi za kisasa, filamu na vipindi vya televisheni, niligundua kwamba tofauti kati ya mtu mwenye furaha, aliyebahatika au anayeishi maisha ya starehe na ilhali kuna ‘ wengine ‘ wanaoteseka kulileta hisia hatia, wasiwasi, usumbufu au aibu.

“Sio kila mtu anahisi kuwa na hatia, lakini wengi wanajisikia wana hatia,” anaongeza Prof Oxfeldt, ambaye amebuni msemo “Scan guilt”.

Maudhui yaliyoagaziwa katika tamthilia za hivi majuzi za Kinorway ni pamoja na washiriki wa “tabaka la starehe ” ambao wanategemea huduma zinazotolewa na wafanyikazi wahamiaji wanaoishi katika vyumba vyao vya chini. Au wanawake ambao wanatambua kuwa wamepata usawa wa kijinsia mahali pa kazi kwa kutegemea wafanyakazi wenye malipo ya chini kutoka nchi maskini kutunza watoto wao, anasema Prof Oxfeldt.

Maisha yana tabia ya kuiga sanaa. Mnamo Machi, serikali ya Norway ilisema ilisimamisha kutoa vibali vya kufanya kazi watu wanaohama kutoka nchi zinazoendelea. Gazeti la udaku la VG lilisema kitendo hicho ni “Mwisho wa utumwa wa magharibi”.

Hisia za hatia za watu wa Norway pia zimechochewa na watu na mashirika mbalimbali yanayotaka kuhoji kama utajiri wa Norway unatokana na shughuli zinazofaanywa kwa njia ya kimaadili.

Mnamo Januari mwaka huu, gazeti la The Financial Times lilichapisha ripoti maalum ambayo ilifichua jinsi mafuta ya samaki yaliyotengenezwa kutoka kwa samaki waliovuliwa katika pwani ya Mauritiania barani Afrika yalivyotumiwa kama chakula na mashamba makubwa ya samaki aina ya chache nchini Norway.

Samaki wa Kinorway wanaofugwa, ambao wanauzwa na wauzaji reja reja barani Ulaya, “wanaathiri usalama wa chakula katika Afrika Magharibi”, gazeti hilo lilisema.

Kikundi cha shinikizo la kimazingira Feedback Global kilisisitiza kuwa “hamu ya kula samaki wa mwituni ya sekta ya Norway inasababisha upotevu wa riziki na utapiamlo katika Afrika Magharibi, na kujenga aina mpya ya ‘ukoloni’ wa chakula”.

Serikali ya Norway ilijibu kwamba ilitaka “kuhakikisha chakula endelevu”, na ilikuwa ikifanya kazi kuelekea “matumizi ya kuongezeka kwa malighafi ya ndani na endelevu zaidi”.

Hakika, Norway inasema ina hamu ya kuendesha mpito kwa uchumi wa kijani, hivyo kuhakikisha ufugaji wa samaki ni endelevu itakuwa muhimu kwani sekta ya mafuta ya petroli inapunguzwa ili kutoa nafasi kwa kinachojulikana kama “mabadiliko ya kijani”.

Hili linafaa kuachilia fedha, teknolojia na nguvu kazi kwa sekta nyingine za baharini ambazo hazina uhakika wa siku zijazo, kama vile nishati ya jua na upepo kutoka pwani, mbali na uzalishaji wa mwani kwa chakula na dawa.

Lakini, kwa sasa angalau, hii haitatosha kuwanyamazisha wakosoaji wakubwa wa tasnia ya mafuta yenye faida kubwa ya Norway. Wanaharakati wa mazingira wanapinga kuendelea kuchimba mafuta na gesi. Wakosoaji wengine wanasema kwamba Norway inategemea sana mapato yake ya mafuta.

Kwa upande mmoja, kutokana na utajiri unaotokana na mafuta na gesi, saa za kazi za Norway zinaelekea kuwa fupi kuliko uchumi mkubwa unaolinganishwa, haki zake za wafanyakazi ni zenye nguvu, na mfumo wake wa ustawi ni wa ukarimu zaidi.

Haishangazi, Norway kwa muda mrefu imekuwa moja ya nchi zenye furaha zaidi ulimwenguni, kulingana na Ripoti ya Ulimwenguni ya Furaha. Kwa sasa iko katika nafasi ya saba.

Lakini kwa upande mwingine, sababu za Børre Tosterud, mwekezaji na mfanyabiashara wa hoteli aliyestaafu, “kutegemea kabisa mapato ya mafuta” kwa Norway kumesababisha bajeti kubwa ya serikali, sekta ya umma iliyo kubwa sana, na uhaba wa wafanyikazi ambao unarudisha nyuma sekta ya kibinafsi.

“Sio endelevu,” anasisitiza.

Norway daima imekuwa ikitazama bahari kwa uchangamfu. Bahari zimekuwa chanzo cha chakula na nishati, mahali pa kazi na kizalishi cha utajiri kwa karne nyingi. Hata hivyo ilikuwa tu mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati ugunduzi wa mafuta na gesi ulisaidia kugeuza utajiri wa taifa hili ambalo hapo awali lilikuwa na maendeleo duni.

Tangu wakati huo, mapato mengi ya mafuta ya Norway yamewekezwa kimataifa na Usimamizi wa Uwekezaji wa Benki ya Norges, ambayo ni sehemu ya benki kuu ya Norway.

Mfuko wake mkuu wa uwekezaji, Mfuko wa Pensheni wa Serikali Global, unaojulikana kama “mfuko wa mafuta”, una mali yenye thamani ya takriban kroner 19,000 ($1,719bn, £1,332bn).

Mapato ya mauzo ya mafuta ya Norway yaliongezeka kufuatia uvamizi wa Urusi wa 2022. Wakosoaji walidai kuwa nchi hiyo ilikuwa ikijinufaisha kutokana na vita hivyo, au angalau kushindwa kushiriki vya kutosha juu ya upepo wake wa ghafla na wahasiriwa wa uchokozi ambao umesababisha.

Waziri Mkuu Jonas Gahr Støre alipuuzilia mbali shutuma za kujinufaisha kwa vita, akipinga kwamba Norway ilikuwa na uwezo wa kusambaza nishati inayohitajika Ulaya wakati wa shida.

Pia anadokeza kwamba Norway imekuwa mojawapo ya wafadhili wakubwa wa kifedha wa Ukraine, na kwa hivyo inapingana kuwa inazidi uzito wake, ikizingatiwa kwamba idadi ya watu wa Norway ni milioni 5.5 pekee.

Jan Ludvig Andreassen anakiri kwamba michango ya Norway nje ya nchi ni “ya kiasi kidogo’

Jan Ludvig Andreassen, mwanauchumi mkuu katika Eika Group, muungano wa benki huru za Norway, anasema kwamba Wanorway “wamekuwa matajiri zaidi kuliko tulivyotarajia”.

Hata hivyo wakati huo huo, anasema kwamba baada ya muda wa viwango vya juu vya riba na mfumuko wa bei unaoumiza, ambao kwa kiasi fulani unasababishwa na krone dhaifu kihistoria, ambayo inafanya bidhaa na huduma zinazoagizwa kuwa ghali, Wanorway wa kawaida hawajioni kuwa matajiri.

Norway pia ni mfadhili anayeongoza duniani wa misaada ya kibinadamu nje ya nchi.

“Nafikiri Wanorwey ni wachangiaji wakarimu wa mambo mazuri,” aonelea Prof Oxfeldt.

Hata hivyo, akizungumzia mauzo ya ziada ya mafuta ya Norway ambayo yametokana na mzozo wa Ukraine, Bw Andreassen anasema kwamba michango ya hisani ya Norway “ni kiasi idogo ikilinganishwa na mapato ya ziada yanayotokana na vita na mateso”. Haya ni maoni yaliyoungwa mkono na Bw Tosterud.

Lakini je, wanakubaliana na Prof Oxfeldt kwamba Wanorway wengi wanahisi kuwa na hatia? “Si kweli, isipokuwa labda katika baadhi ya duru kama vile harakati za mazingira,” anasema Bw Andreassen.

Bw Tosterud anakubali. “Sina hisia yoyote ya hatia, na sidhani kama imeenea nchini Norway.”

About The Author

Gate of Wise

Gate of Wise empowers you to stay ahead in digital innovation with insightful and accurate news on AI, blockchain, and digital currencies. We also offer smart advertising solutions to seamlessly connect your brand with a tech-savvy and engaged audience.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Next Post

SOBANUKIRWA IMIRIMO ITSINDA RIYOBOYE PI NETWORK KU ISI BAHUGIYEMO MBERE Y’IFUNGURA RY’UMUYOBORO (OPEN MAINNET)

Mon Jul 29 , 2024
Mu iterambere ryibanze rinyeganyeza isi y’ifarangakoranabuhanga(crypto world), Pi Network imaze kugera ku ntera ishimishije hamwe no gusinya amasezerano 219 yo gutanga umutungo (SACs) kurubuga rwa Stellar. Iyi ntambwe yerekana ko ibihugu 219 byatangije uburyo bukenewe cyane (HDTM) ku mutungo wabyo ku muyoboro wa Pi. Ibi byagezweho ntabwo byagura Pi Network […]

You May Like

Breaking News